Ezekiel 18:1-6

Roho Itendayo Dhambi Itakufa

1Neno la Bwana likanijia kusema: 2 a“Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli: “ ‘Baba wamekula zabibu zenye chachu,
nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’?

3 b“Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli. 4 cKwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.
5 “Mtu aweza kuwa ni mwenye haki
atendaye yaliyo haki na sawa.

6 dHakula katika mahali pa ibada za miungu
kwenye milima
wala hakuziinulia macho sanamu
za nyumba ya Israeli.
Hakumtia unajisi mke wa jirani yake,
wala hakukutana kimwili na mwanamke
wakati wa siku zake za hedhi.
Copyright information for SwhKC